HABARI MPYA

Tuesday, November 25, 2014

KINANA ATINGA MASASI, ATAKA CCM IENDELEE KUIBANA SERIKALI JUU YA WAFUJAJI WA FEDHA ZA UMMA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi na kuwaambia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi alisema lazima tutangulize utumishi kwa umma.
 Kadi zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama cha NLD Taifa Ndugu Frank Rashid Maulano aliyejiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi.
Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
 Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Marika wilayani Masasi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Marika ikiwa sehemu ya kujenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi ambapo alikagua maendeleo ya mradi wa maji wa Chiungutwa mradi ambao utasaidia vijiji 27,tarafa 3 ambapo watu zaidi ya elfu 60 watanufaika na mradi huo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa wilaya ya Masasi ambapo aliwapongeza kwa kutambua utapeli wa vyama vya upinzani katika kijiji chao na kuamua kujitenga nao kabisa.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa ambapo aliwapongeza kwa kuwa na Mbunge mchapa kazi anayejali wananchii wake,Kinana aliwaambia wananchi hao wahakikishe wanajiandikisha tayari kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
 Mbunge wa Jimbo la Lulindi ( CCM ) Jerome Bwanausi akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa na kuwaeleza maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwenye jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mbunge wa zamani wa mkoa wa Mtwara John Aidi aliyekuwa mbunge wa Mtwara miaka ya 75 mpaka 85 na aliwahi kuwa mbunge wa Masasi miaka ya 65 mpaka 70 akifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

No comments:

Post a Comment